Ushindi dhidi ya Mbao FC

1200X600 SE

Mchezo nambari 161 wa ligi kuu soka Tanzania bara umemalizika katika dimba la Sokoine leo hii, Mbeya City ikitumia faida ya uwanja wa nyumbani kujikusanyia alama tatu muhimu dhidi ya Mbao FC kutoka Mwanza.

Mchezo uliokua na kasi na upinzani mkubwa toka kwa timu zote mbili. Dakika ya 30 ya mchezo beki wa kulia John Kabanda akafunga goli la kuongoza baada ya mlinda mlango wa Mbao kuutema mpira mita kadhaa kutokea langoni mwake. Hadi dakika 45 za kipindi cha mwanzo zinakamilika, City alikua akiongoza kwa goli 1 dhidi ya Mbao FC. Mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza, Eliud Ambokile aliongeza goli la pili kwa mkwaju wa penati iliyotokana na beki wa Mbao FC kuunawa mpira katika lango lake.

Hadi dakika 90 zinakamilika, City aliongoza kwa magoli 2 dhidi ya 1 la Mbao FC.

Baada ya mchezo huu, klabu inasafiri kwenda Mabatini huko Mlandizi kucheza na Ruvu Shooting. Huu utakua mchezi nambari 172 wa raundi ya 22 katika ligi. Baada ya raundi hii ya 21 City inapanda mpaka nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi ikiwa imekusanya jumla ya alama 24.

Imeandikwa na
Shah Mjanja

Afisa Habari.

 

Video: Mazoezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *