UMOJA WA MASHABIKI WATEMBELEA MAZOEZI

1200X600 SE

Kikosi cha timu yetu pendwa leo hii tarehe 25 Januari kimefanya mazoezi  ya mwisho katika dimba la Sokoine Jijini Mbeya kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar kutoka Manungu Morogoro.

Mchezo huu utachezwa katika dimba la Sokoine majira ya saa 10 jioni siku ya Jumamosi tarehe 27 Januari. Mpaka sasa hakuna majeruhi , lakini mandalizi yamekuwa mazuri sana, kikosi chote na benchi la ufundi wana morali ya juu.

Katika mazoezi ya leo timu ilitembelewa na viongozi wa matawi ya timu, lengo lilikuwa ni kutoa motisha kwa wachezaji wetu na kuwapa moyo pamoja na kuwakikishia kuwa wana imani timu itafanya vizuri licha ya kuwa tunapitia katika kipindi kigumu.

Mashabiki wamesisitiza ushirikiano wa timu na wameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kwenye timu, na kikao hiki kimekua chenye maono chanya na kimefungua kurasa mpya kati ya mashabiki wetu na wachezaji. Pia, wachezaji pamoja na benchi la ufundi walitoa maneno ya shukrani kwa kutembelewa na viongozi wa matawi ya Mbeya City Fc na kuahidi kupambana zaidi.

Endelea kununua jezi na bidhaa za timu, na kufika uwanjani ili tuipe nguvu timu yetu.

Imeandikwa na

Daniel Mwakasungula

Fasiliti ya Habari za Klabu

Video: Training Session 25.01.18

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *