TUPO SONGEA MJINI

DCIM100MEDIADJI_0078.JPG

Kikosi chetu chenye wachezaji 25 na watumishi 12 kimesafiri leo hii alfajiri kuelekea Songea Mjini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Majimaji.

Huu utakua mchezo wetu wa kwanza wa duru la pili baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar wiki iliyoisha.

City inakutana na Majimaji baada ya kuifunga goli 1 kwa sifuri katika mchezo wake wa kwanza uliochezwa dimba la Sokoine 26.08.17 na kuibuka na ushindi.

Baada ya mchezo huu wa Majimaji 03.02.18 klabu itasafiri kuelekea Mtwara kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda na kisha kurejea Njombe Mjini kucheza na Njombe Mji.

Natoa wito kwa mashabiki waliopo maeneo hayo yote kufika kwa wingi viwanjani, huku wakiwa wamevalia jezi zetu nzuri za rangi ya dhambarau au hizi nyeupe; na kuipa nguvu timu yetu pendwa.

Shabiki mmoja alisema ‘Mambo yote yatapita na City itasimama’, tunaendelea kupambana kwa nguvu moja, imani na mafunzo makubwa na tutafanya vizuri zaidi katika duru hili la pili.

Shah Mjanja
Afisa Habari

Tazama matukio katika mechi yetu dhidi ya Mtibwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *