TUMEPOTEZA MCHEZO

1200X600 SE

Umekua mchezo mgumu dhidi ya Yanga SC. Matokeo ya mchezo wa leo yametuumiza sana hasa ukizingatia tutakua tumepoteza mechi 3 mfululizo. Benchi la ufundi linatekeleza wajibu wake wa kukinoa na kutoa mafunzo ya kiufundi ili kuwa na kikosi imara zaidi.

Tuna imani michezo ijayo tutafanya vizuri zaidi na kujiweka katika nafasi bora ya ushindani. Napenda kuwapa pole mashabiki na wapenzi wote wa klabu hii pendwa, umoja na mshikamano wetu ni muhimu zaidi na siku zote tutaendelea kuipa nguvu Mbeya City FC.

Shah Mjanja
Ofisa Habari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *