Tanga Raha…

Wami

Kikosi chenye wachezaji 22, benchi la ufundi 08, idara ya habari na madereva 02 kimesafiri kutoka Mbeya na kuwasili jioni ya leo tarehe 14.11.17 katika mji wa Tanga, umbali wa kilomita 1100 kutoka Mbeya mjini.

Tanga ni mji wa mwambao, wenye wapenzi wengi wa soka na mashabiki waaminifu wa Mbeya City Fc. Ni mji wa Binslum Tyres Company Limited, ambaye ni mdhamini rasmi wa klabu yetu pendwa kupitia bidhaa yake ya RB Battery.

Hapa Tanga tutafanya mazoezi katika viwanja mbalimbali ukiwemo uwanja wa Mkwakwani katika maandalizi yetu ya kila siku chini ya Mwalimu Nsanzurwimo Ramadhan. Siku ya jumatano tarehe 15.11.17 tutakua na mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya soka ya Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani majira ya saa kumi jioni.

Pia, klabu yetu itautumia mji wa Tanga kama sehemu ya maandalizi yake kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu unaofuata dhidi ya Yanga SC ya Dar es Salaam. Tunatazama kwa ufahamu, imani na matumaini kuwa Tanga patakua mahala sahihi na matayarisho yetu ya ligi kuu.

Shah Mjanja
(@shahmjanja)
Ofisa Habari
MCCFC
717-282-217

VIDEO – Mazoezi Sokoine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *