TAARIFA

1

Klabu imeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya @officialsingidaunitedfc utakaochezwa katika uwanja wa NAMFUA huko Singida mwishoni mwa wiki hii. Mchezo huo wa ligi kuu utakua ni wa raundi ya 11 na kisha kufuatiwa na mapumziko ya ligi kupisha michuano ya Chalenji.

Kocha Mkuu Mwl. Ramadhan anayatumia mazoezi kama ilivyo ratiba na kazi za kila siku ikiwemo marekebisho ya mapungufu katika sehemu zilizo na uhitaji.

Leo asubuhi tulifanya vikao, screening (utazamaji wa mechi za awali), na darasa la kiufundi yaani Master-Class. Lengo la vikao hivi na mafundisho haya ni sehemu ya mafunzo kwa klabu na yenye nia ya kujiboresha na kuongeza ufanisi hasa baada ya kupoteza michezo 3 mfululizo. Mchana timu ilishiriki mazoezi katika uwanja wa chuo cha Jordan hapa Morogoro mjini.

Pia, kama ambavyo wengi wanauliza; Owen Chaima alipewa adhabu ya kusimamishwa kucheza ligi kuu tarehe 04.11.17 kwa kosa la tarehe 27.10.17 wakati wa mechi dhidi ya Azam FC. Yaani alisimamishwa kucheza ligi siku tisa (9) baada ya kosa hilo na ambayo ni siku moja (1) kabla ya mchezo wa tarehe 05.11.17 dhidi ya Simba.

Pengo la Owen Chaima limechangia kudhoofisha klabu yetu na tuna amini sasa, pengine baada ya mechi ya Singida atapewa hukumu na tutafahamu hatma yake.

Klabu inawapa pole wapenzi mashabiki wa timu hii pendwa kwa matokeo yasiyoridhisha. Tunaendelea kusonga mbele kwa imani kubwa (presumption of good faith) huku tukizingatia taaluma, nafasi, mazoea na wajibu wetu katika Soka.

Tulipata majeruhi katika mchezo dhidi ya Yanga, na michezo iliyopita. Haruna Shamte, John Kabanda, Ally Lundenga, Eric Kyaruzi na Emanuel Kakuti aliyeumia katika ushiriki wake Taifa U23. Wachezaji hawa wameonesha muitikio mkubwa katika tiba inayotolewa na wataalamu wetu na tuna imani watatumika katika mchezo ujao.

Mbolea ya shamba ni miguu ya mwenye shamba… Tutapambana na uhitaji wetu tutajitimizia sisi wenyewe.
Mbeya City FC is inclusive, tunataka kila mtu ashiriki katika hatua muhimu na unaweza kutuandikia kupitia info@mbeyacityfc.com au fika katika ofisi za klabu zilizopo mtaa wa Sisimba ukumbi wa Mkapa.

Imetolewa na
Shah Mjanja (@shahmjanja)
Fasiliti ya Habari za klabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *