SHINYANGA: TUMEFIKA

1200X600

Kikosi cha Mbeya City FC kimewasili mjini hapa na kuweka kambi rasmi yenye mafunzo mahususi chini ya Mwalimu Kijuso ambaye rekodi yake msimu huu imeanza vema. Tupo hapa tayari kupambana dhidi ya mwenyeji wetu Stand United hapo jumapili katika uwanja wa Kambarage.

Ilikua safari ya masaa mengi kutoka Mbeya kupitia Iringa, Dodoma, Tabora mpaka Shinyanga mjini; takribani kilomita 1166 ndani ya basi letu la kisasa na lenye nakshi za kifalme kwa ajili ya wachezaji wetu, benchi la ufundi na maafisa wa klabu yetu.

Tukiwa njiani kutoka Dodoma kuelekea Nzega tulifanya kikao katika sehemu ya mikutano iliyo nyuma ya basi letu huku tukitazama mandhari nzuri ya nchi hi kupitia vioo vyenye ‘tinted’ nyepese vya MCC ONE basi hili la kisasa kabisa. Kikao hicho kilihudhuriwa na Kocha msaidizi Mohamed Kijuso, Meneja Geofrey Katepa, Kepteni Mwasapili na Sankhani. Pamoja nao alikuwepo pia Kit Man wa klabu Rashid Kasiga na Kocha wa Makipa Josia Steven huku kalamu za www.mbeyacityfc.com zikishikwa na Mwanahabari Shah Mjanja.

Kikao hicho kilikua ni kuupitia mpango mkakati na mbinu ya mashambulizi kwa ajili ya kuwaua wapiga debe wa Stand United siku jumapili katika uwanja wao wa Kambarage.

Mara baada ya kikao hicho tulishushia maji ya Dasani, bidhaa bora kabisa ya Cocacola ambaye ni mdhamini wetu huku miondoko tulivu ya kifalme ya basi hili aina ya Aero Queen MV ikituvuta na kutuwezesha kuiona Tanzania kwa uzuri kabisa.

Unaweza kutazama picha zaidi zilizopigwa na mpiga picha wetu Hassan katika ukurasa wetu wa instagram.

Hadi hapo jumapili katika uwanja wa Kambarage,

 

Sauti: Taarifa kwa sauti hapa chini

Wasalaam.

Shah Mjanja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *