POINTI 11

1200X600 SE

Mchezo nambari 52 wa ligi Kuu Tanzania bara uliotukutanisha na Ruvu Shooting umemalizika kwa ushindi wa magoli 2 kwa sifuri dhidi ya wapinzani wetu Ruvu Shooting ya Pwani. Ulikua mchezo mgumu kwa sababu wapinzani wetu wamekua na matokeo mabaya katika ligi kuu mpaka sasa, lakini uimara wa vijana wetu uliweza kutupatia ushindi mnono usio na mashaka.

Magoli yetu yalifungwa dakika ya 36 na 52 na Eliud Ambokile na Frank Hamis. Katika mchezo huu golikipa wetu nambari moja Owen Chaima hakuruhusu goli hata moja katika wavu wake. Eliud Ambokile anafikisha idadi ya magoli 4 katika ligi kuu na hii inampatia nafasi ya kuwa miongoni mwa wafungaji 10 bora wa ligi mpaka sasa baada ya mechi ya raundi ya saba kuisha.

Matokeo ya mchezo huu yanatupeleka nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wiki hii na mchezo wetu unaofuata ni dhidi ya Azam FC katika dimba la Chamazi, mchezo huo wa ligi nambari 57 utachezwa majira ya saa moja usiku kwa saa za afrika ya mashariki.

Mungu Ibariki Mbeya City.

Shah Mjanja
Afisa Habari
0623 154 077

Table Week 7

VODACOM PREMIER LEAGUE 2017-2018

PosTeamPWDLFAGDPts
111650236+1723
21165093+623
311560175+1221
41155195420
51146185+318
611362119+215
71135388014
8112541112-111
911254911-211
101125479-211
111125468-211
12113261016-611
1311254615-911
1411155916-69
1511155411-78
1611146311-87

Video: Press Conference (20.10.17) ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *