POINTI 1 MWADUI

1200X600

Ligi soka nchini imeendelea katika raundi ya 5  Mbeya City ikishuka dimbani kuvaana na Mwadui ya Shinyanga. Klabu yetu iliingia katika mchezo huo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Stand United katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Mchezo huo nambari 37 wa ligi kuu soka Tanzania bara uliochezwa katika uwanja wa Mwadui huko Shinyanga ulimalizika kwa sare ya magoli 2 kwa 2.

Kikosi kilichoanza katika mchezo huo kilikongozwa na kepteni Sankhani Mkandawile  na nyota Owen Chaima, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Erick Kyaruzi, Ally Lundenga, Mrisho Ngassa, Mohamed Samata, Frank Hamis, Mohamed Mkopi na Eliud Ambokile.
Wachezaji wa akiba wakiwemo Fikirini Bakari, Haruna Shamte, Medson Mwakatundu, Idd Seleman, Victor Hangaya, Babu Ally na Omary Ramadhani.

Mwalimu Kijuso alifanya mabadiliko dakika ya 48 na 49 yaliyowaingiza Babu Ally na Idd Seleman waliochukua nafasi ya Ally Lundenga na Mrisho Ngassa, na kisha baadae dakika ya 63 Victor Hangaya aliingia kuchukua nafasi ya Frank Hamis ‘Ikobela’.

Magoli yetu yalifungwa na Mohamed Samata dakika ya 01 ya mchezo na kisha Mohamed Mkopi dakika ya 78. Goli la Mohamed Samata linabaki kuwa goli la mapema kabisa katika ligi kuu mpaka sasa.
Katika mchezo huo Kepteni Sankhani Mkandawile alipata kadi ya njano.

Kikosi kitaendelea kuwepo hapa Shinyanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Mbao utakaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba tarehe 13.09.17. Mbeya City FC itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga mbao katika uwanja huo huo magoli 1-4.

Mungu Ibariki Mbeya City FC.

Shah Mjanja
Afisa Habari
0717282217

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *