NURU ORPHANAGE CENTRE

1200X600 SE

Klabu yetu leo hii jioni ilitembelea kituo cha watoto yatima cha Nuru Orphanage Centre kilichopo Uyole hapa jijini Mbeya. Tuna amini watoto hawa ni mashabiki wetu na hapo baadae wanaweza kuwa wachezaji, madaktari au walimu wa klabu hii pendwa.

Kocha mkuu Ramadhan Nsanzurwimo na benchi lake, wachezaji, watumishi na idara ya habari ni sehemu ya waliofika katika kituo hiki.

Hii ni sehemu ya uwajibikaji wetu katika makundi maalumu ndani ya jamii yetu. Tumefurahi sana kuwa nao na hasa malezi bora wanayopata toka kwa walezi wao.

Tutaendelea kuunga mkono makundi yote yenye uhitaji katika jamii na kufurahi pamoja.

Mbeya City FC.

Shah Mjanja
Afisa Habari

Video: Mashabiki wa Mbeya City watembelea kituo cha watoto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *