‘NI FAINALI’ KESHO DHIDI YA LYON

dsc_0102

KIKOSI cha Mbeya City fc  kesho kinashuka kwenye uwanja wa Sokoine kucheza mchezo wa 28 wa ligi kuu ya vodacom  Tanzania  bara dhidi ya wageni African Lyon kutoka jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa kikosi hicho Mohamed Kijuso amesema  mchezo huo dhidi ya Lyon wanauchukulia kama fainali ya kutokana na uwepo wa umuhimu mkubwa wa kushinda  kufuatia matokeo mabaya kwenye michezo  miwili iliyopita

Kesho tunakwenda kucheza mchezo muhimu pengine kuliko yote tuliyocheza kwenye duru hii ya pili, tunahiaji kushinda ili kujiweka kwenye nafasi nzuri, hatukuwa na matokeo mazuri kwenye mechi mbili zilizopita,ulikuwa wakati mgumu  kwetu lakini, tumerekebisha makosa sasa tunakwenda kucheza mchezo muhimu ambao ni kama fainali kwetu kwa sababu hatuhitaji jambo lingine zaidi ya pointi tatu baada ya dakika 90.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *