NAMFUA STADIUM SINGIDA

1200X600 SE

Kikosi cha Mbeya City FC kimewasili mjini Singida siku ya alhamisi tarehe 23.11.17 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo nambari 82 wa jumamosi (25.11.17) dhidi ya Singida United. Kikosi hiki kiliendelea na mazoezi katika viwanja vya Jordan na Highland Camp huko Morogoro.

Mchezo huu utakua ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi kukutana mara baada ya Singida United kupanda daraja msimu huu wa 2017/2018.

Mara baada ya mchezo huu timu itarejea nyumbani kupisha mapumziko ya Kilimanjaro Heros itakayoshiriki mashindano ya Chalenji huko Kenya.

Mchezo unaofuata baada ya Singida United ni dhidi ya Kagera Sugar, mchezo wa ligi nambari 90 katika dimba la Sokoine.

 

Shah Mjanja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *