Mwamuzi J. Adongo aikoa Ruvu Shooting

1200X600 SE

Dakika 90 za mchezo wa ligi nambari 172 wa raundi ya 22 uliotukutanisha na Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini hapa Mlandizi zimemalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili. Klabu yetu iliyokua makini kwa wakati wote wa mchezo ilifanikiwa kufunga magoli ya kuongoza huku tukiwaacha wapinzani wetu nyuma kwa kandanda safi, ufundi wa hali ya juu na mpira wa nidhamu.

Eliud Ambokile ndiye aliyekua wa kwanza kuaindikia City goli la kuongoza dhidi ya Ruvu Shooting, goli hilo lilitokana na shuti kali la Frank Hamis lililomlenga mlinda lango wa Ruvu Shooting; ambaye alishindwa kuhimili na kuuachia mpira uliowekwa wavuni na Eliud mnamo dakika ya 15 ya mchezo.

Dakika ya 52 ya mchezo, baada ya Ruvu Shooting kupiga penati yao, vijana wetu machachari walifanya ‘kaunta attack’ ya nguvu na Frank Hamis kufanikiwa kuongeza goli la pili.

Eliud Ambokile amefunga jumla ya magoli 10 katika ligi Kuu na anaingia katika vinara watatu wenye magoli mengi katika ligi Kuu akiwa nyuma ya Emanuel OKwe (Simba) na Obrey Chirwa (Yanga).

Mwamuzi Jacob Adongo, ambaye tangu mwanzo wa mchezo alishindwa kutafasiri sharia 17 za mchezo huu vizuri alichangia sana kupunguza nguvu za vijana wa City, yeye pamoja na Mwamuzi msaidizi nambari moja walionesha dalili za kuzidiwa nguvu na mchezo huu na kufanya maamuzi ambayo hayakua sahihi hasa kwa upande wetu. Dakika zote tulishuhudia ‘offside’ nyingi zisizo halali pale vijana wetu walipoonekana mwiba langoni mwa Ruvu Shooting, na kwa mashaka palikua na ‘offiside’ tele halali za Ruvu Shooting langoni mwetu ambazo zilifanywa kuwa sahihi. Hii ilitupunguzia kasi ya mchezo na kubinya nafasi yetu ya ushindani.

Kulikua na faulo nyingi za wachezaji wa Ruvu Shooting ambazo zilikua na faida kwetu lakini mwamuzi alisimamisha mpira. Karaha hii na maamuzi ya shaka ndiyo yalioisaidia Ruvu Shooting kupata goli la kwanza dhidi yetu.

Mnamo dakika za mwisho za mchezo huu, mara baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika mwamuzi aliongeza dakika 6 za ziada; dakika hizo ziliisha na mchezo kiuendelea kwa dakika 12 zaidi baada ya dakika 90 mpaka hapo Ruvu Shooting walipopata goli la kuotea na mwamuzi kumaliza mpira mara moja.

Klabu inasikitishwa na maamuzi mengi yasiyozingatia sharia za mpira na ambayo moja kwa moja yametuondolea nafasi sawa ya ushindani katika ligi Kuu.

Mchezo wetu unaofuta tutacheza na Azam FC katika dimba la Sokoine 04.04.18 majira ya saa kumi za jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Kikosi chetu chenye wachezaji 22, benchi la ufundi 6, Idara ya Habari 4 na watumishi wengine kinataraji kuondoka alfajiri ya kesho na kurejea nyumbani Mbeya.

Imetolewa na

Afisa Habari

Mbeya City FC.

Video: Mazoezi Sokoine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *