Urafiki Mwema na Coastal Union

1200X600 SE

Dakika 90 zimekamilika kwa matokeo ya goli 2 – 2 dhidi ya Coastal Union ya hapa Tanga inayoshiriki ligi daraja la kwanza. Magoli yetu yakifungwa na Frank Hamis na Omary Ramadhani.

Mbeya City FC  imewahi kukutana na Coastal Union mara kadhaa katika michezo ya ligi kuu soka Tanzania bara kabla ya Coastal kushuka daraja. Mchezo huu wa kirafiki umefanyika kwa lengo la kuwapa burudani wakaazi wa mji huu ambao walijitokeza kwa wingi kuzitazama timu zao pendwa.

Mwalimu Ramadhani aliutumia mchezo huu kuwatazama nyota kadhaa waliofika kufanya majaribio katika klabu yetu.

Shah Mjanja
717-282-217

 

Video – Mapara na Bab Ally

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *