MAY 13 DAR,MAANDALIZI YANAENDELEA

20170125_103606

SIKU moja baada ya kurejea  jijini Mbeya kutoka Sumbawanga kilipokuwa kimeweka kambi ya siku tano na kucheza michezo minne ya kirafiki ikiwa ni matayarisho ya mchezo uajo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania bara dhidi ya Young African May 13 jijini Dar, kikosi cha Mbey City fc  leo kimeenelea na mazoezi kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari  igawilo jijini hapa.

Meneja wa kikosi hicho Geofrey Katepa ameidokeza mbeyacityfc.com kuwa  hali za nyota wote kikosini ni njema kabisa na maandalizi ya mchezo wa May 13 yanakwenda vizuri huku morali ya kikosi ikiwa juu hasa baada ya ushindi kwenye michezo minne ya kirafiki na mabingwa wa mkoa wa Rukwa.

Tulicheza michezo minne ya kirafiki Sumbawanga, tulifanikiwa kushinda yote,hili limetuongezea morali kubwa kueleka mchezo dhidi ya Young Africans  kwenye uwanja wa Taifa,kikosini hakuna majeruhi yeyote na tunajipanga kuhakikisha tunashinda mchezo huo, wapinzani wetu tunawajua wana timu nzuri na ngumu lakini soka linaweza kukupa matokeo sehemu yoyote  hivyo tuko tayari kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha tunapata matokeo dhidi yao hapo May 13.

  Picha/video zaidi fungua hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *