MATOKEO MABAYA MCHEZO WA MWISHO

NF6_9574

BAO la dakika  ya  78  la Omary Ramadhani  lilishindwa kuikoa City ugenini baada ya kuhitimisha dakika 90 ikiwa nyuma kwa bao 2-1 dhidi ya weenyeji Majimaji Fc katika mchezo wa mwisho  wa kufungia msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bar  uliochezwa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea jumamosi iliyopita.

Yakubu Kibiga alianza kuifungia Majimaji bao mapema kipindi cha kwanza kufuatia shuti kali la dakika ya 43 akimalizia kazi nzuri ya Kelvin Sabato aliyefanikiwa  kuutuliza mpira vizuri akiwa karibu na lango kisha kutoa  pasi kwa mfungaji aliyekuwa akimtizama mlinda lango Owen Chaima  kisha kuukwamisha wavuni.

Baada ya mapumziko City ilirudi vizuri na kuanza kulishambulia lango la Majimaji kwa mashambulizi ya mara kwa mara yaliyokuwa yakijengwa vyema kutokea eneo la katikati lililokuwa likiongozwa na Raphael Daud na Kenny Ally, na baada ya dakika kadhaa za kucheza soka la uhakika Omary Ramadhani aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Rajabu Isihaka alifanikiwa kukwamisha mpira wavuni baada kipa Hashimu Mussa kushindwa kuthibiti shuti la Hassan Mwasapili na mpira kumfikia mfungaji.

Mara baada ya Mchezo kocha kinnah Phiri alionekan kutokuridhishwa na matokeo hayo licha ya kuwsifu vijana wake kwa kuonyesha kandanda safi muda wote wa kipindi cha pili.

Tulikuwa na changamoto ya kuuzoea uwanja, hii ndiyo sababu hatukucheza vizuri kipindi cha kwanza, tulivyorudi vyumbani tulilizungumza hili na kupanga mbinu mpya,tulifanikiwa kuwathibiti dakika zote 45 za pili, lakini hii ni soka baada ya dakika 90 matokeo yamekuwa hivyo, hatujafurahishwa nayo kwa sababu heshima yetu ilikuwa kwenye kushinda mchezo.

NF6_9534
Rajab Isihaka (katikati) akijaribu kuwatoka walinzi wa Majimaji Fc kwenye mchezo wa VPL uliochezwa jumamaosi uwanja wa Majimaji na City kupoteza 2-1

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *