MATCH DAY 3 – Na Njombe Mji

1200X600

Kikosi cha Mbeya City FC kinashuka tena dimbani leo hii 17.09.17 katika uwanja wa sokoine kuikabili timu ya Njombe Mji kutoka Mji wa Njombe, mtanange utakaorushwa moja kwa moja kupitia kituo cha matangazo cha Azam TV kuanzia majira ya saa kumi kamili jioni kwa saa za Afrika ya mashariki.

Mchezo huu namba 23 wa ligi kuu soka Tanzania bara utaambatana na mchezo mwigine nambari 24 utakaozikutanisha Simba SC na Mwadui FC katika uwanja wa Taifa huko Dar es Salaam. City inaingia uwanjani ikitokea nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi baada ya michezo yote ya raundi ya pili kukamilika. Alama tatu katika mchezo wa leo zitaipeleka City katika nafasi ya 4, 5 au  6 kulingana na msimamo wa ligi baada ya mechi hizi xs raundi ya tatu kukamilika.

Meneja wa timu Mr. Godfrey Katepa ameihakikishia mbeyacityfc.com kuwa kikosi chote kipo kamili na tayari kwa mpambano. ‘Timu yetu iko safi kabisa, wachezaji wako kamili kupambana na sisi kama benchi la ufundi tumejiandaa kwa pamoja kuchukua pointi 3 muhimu. Napenda kuwaambia mashabiki na wapenzi wa timu yetu wafike kwa wingi; kushuhudia kabumbu safi linalovutia toka Mbeya City.’

Kikosi kinachopambana leo kitaongozwa na kepteni Sankhani Mkandawile na wachezaji wafuatao watakua katika mchezo.

1. Oweni Chaima

2. Haruna Shamte

3. Hassan Mwasapili

4. Erick Kyaruzi

5. Sankhani Mkandawile

6. Ally Lundenga

7. Eliud Ambokile

8. Mohamed Samata

9. Frank Hamis

10. Mrisho Ngasa

11. Mohamed Mkopi

SUB

Fikirini Bakari

John Kabanda

Babu Ally

Ramadhani Malima

Anthony Mwingira

Idd Seleman

Victor Hangaya

————–
Shah Mjanja
@shahmjanja

MCCFC

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *