MAGOLI 7 DHIDI YA MBAO FC…

1200X600

Ligi Kuu Tanzania bara raundi ya 6 inaendelea tena wiki hii katika viwanja mbalimbali nchini na mchezo nambari 41 utatukutanisha na Mbao FC ya jijini Mwanza. Mchezo huu utakaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba utahitimisha mechi zetu tatu za mwanzo za ugenini baada ya zile za Stand na Mwadui katika kanda ya ziwa.

Mbeya City FC inaingia katika mchezo huu ikiwa na rekodi ya kuifunga timu hiyo mpya katika ligi ya Tanzania bara nyumbani na ugenini. Msimu uliopita mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba Mbeya City FC iliibuka na ushindi wa magoli 1-4, magoli hayo yakifungwa na Ramadhani Chombo ‘Redondo’, Rafael Daud na Omary Ramadhani. Duru la pili katika uwanja wa Sokoine kwa mara ingine tena Mbeya City iliibuka na ushindi mwingine wa magoli 3-1, magoli yaliyowekwa wavuni na Zahoro Pazzi, Tito Okelo na Rafael Daud.

Rekodi hii ya magoli 7 kwa 2 dhidi ya mbao inaiweka klabu yetu katika nafasi kubwa zaidi ya kushinda mechi hii itakayochezwa hapo kesho (13.10.17) majira ya saa kumi jioni; mchezo utakaorushwa na kituo cha matangazo cha Azam TV.

Meneja wa Timu Geofrey Katepa amezungumza na www.mbeyacityfc.com kuelekea mchezo huo hapo kesho ‘Tumefika salama jijini Mwanza, hali ya hewa imepoa na hakuna joto sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Tunatazama kuwa na mchezo mzuri hapo kesho maana kikosi chote kiko ‘fiti’ na hatuna majeruhi kabisa’.

Kocha Ramadhani anakwenda kuongoza mchezo wake wa kwanza akiwa na kikosi cha dhambarau kutoka Jijini Mbeya na hii itakua mechi yake ya kumbukumbu katika soka la Tanzania.

Mchezo utaofuata baada ya huu wa Mbao FC utachezwa katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya dhidi ya Ruvu Shooting tarehe 21.10.17.

Mwenyezi Mungu aibariki Mbeya City FC.

Video: Happiness na Doris Mashabiki wa mbeya CIty Mwanza

Shah Mjanja
Afisa Habari
0623 154 077

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *