MABADILIKO BENCHI LA UFUNDI

1200X600 SE

Klabu ya Mbeya City FC leo hii imefanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi kutokana na uhitaji na nafasi; mabadiliko haya yanahusisha nafasi ya Kocha Msaidizi, Meneja wa Timu na Mtunza vifaa.

Mwalimu Mohamed Kijuso amerejea katika timu yake ya awali (Timu B) na ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo yenye nyota wachanga. Timu hii ya vijana imekua lishe kwa timu kubwa na tuna imani itasaidia kuongeza ushindani katika kikosi chetu. Mwalimu Josiah Steven ambaye ndiye kocha wa magolikipa wa Mbeya City FC anakaimu nafasi ya Kocha msaidizi.

Godfrey Katepa aliyekua meneja wa timu na Rashid Kasiga aliyekua mtunza vifaa wa klabu, wamemaliza mikataba yao na klabu yetu. Klabu itatangaza watumishi watakaochukua nafasi zao.

Imetolewa na
Shah Mjanja

0717282217

 • Mwakajange January 12, 2018 at 11:34 pm

  I need the old white Jersey ?
  Can I get it

  • Shah Mjanja March 2, 2018 at 12:19 pm

   Hello Mwakajange,
   We do not have those jersey on stock, however -we are noticing that some vendors in streets (Mbeya) are still selling them. We advice you to do a window shopping in those Mbeya Streets.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *