KWAHERI RUVUMA

1200X600 SE

Dakika 90 zimemalizika hapa mkoani Ruvuma katika wilaya ya Mbinga baada ya City kuibuka na ushindi wa magoli 3 kwa 1 dhidi ya mwenyeji wetu Mbinga United. Mchezo ulioshihudiwa na wakaazi wengi wa wilaya hii akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Ndugu Cosmas Nshenye, Katibu Tawala na wakurugenzi wa wilaya ya Mbinga Mjini na Mbinga Vijijini.

Mchezo huu unahitimisha mechi nne za kirafiki tulizocheza katika mkoa huu wakati huu wa mapumziko kupisha mashindano ya kombe la Mapinduzi huko Zanzibari.

Matokeo katika michezo hii minne
1. City ilishinda goli 4 kwa sifuri
2. City ilishinda goli 2 kwa sifuri
3. City ilishinda goli 5 kwa sifuri
4. City ilishinda goli 3 kwa 1

Baada ya mechi hii ya leo tunarejea nyumbani Mbeya kwa ajili ya mchezo unaofuta wa ligi kuu dhidi ya Prisons SC hapo tarehe 14.01.18

Shah Mjanja
Afisa Habari

Video: Shabiki wa Mbeya City kutoka Botswana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *