KINNAH:TUMESIKITISHWA,NAFASI BADO TUNAYO

img_0983

KOCHA mkuu wa kikosi cha Mbeya City Fc  Mmalawi Kinnah Phiri amesema  amesikitishwa na matokeo yaliyopatika kwenye michezo miwili ya ligi kuu Tanzania bara iliyochezwa  kwenye uwanjani wa Sokoine jijini hapa jumamosi iliyopita na jana jumatano.

Akizungumza na mbeycityfc.com muda mfupi uliopita kocha Phiri ameweka wazi kuwa mipango iliyokuwepo kabla ya michezo hiyo miwili kuchezwa ilikuwa ni kushinda ili kukusanya pointi ambazo zitaiweka timu katika nafasi nzuri zaidi kwenye msimamo wa ligi  iliyo ukingoni hivi sasa.

Soka ni mchezo wa ajabu ziko nyakati ambazo unakupa matokeo usiyoyatarajia,tulijiandaa vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,tulijua umuhimu wa kushinda michezo hii  miwili,mapema tulihitaji kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya mechi zinajazo,hayo yote hayakutokea inasikitisha kuona tumevuna pointi mbili pekee kati ya sita zilizohitajika, hakuna namna nyingine, huu ndiyo mpira wa miguu ni laziama uheshimiwe.

Akiendelea zaidi kocha Phiri  alisema pamoja na matokeo hayo ya kupata pointi mbili kufuatia sare dhidi ya Ruvu Shooting  pia Mtibwa Sugar,nafasi ya City kuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu bado ipo japo inahitaji kuongeza nguvu na kujitum zaidi ili kufanikisha matokeo kwenye mechi zinafuata ikiwa ndiyo jambo pekee linalohitajika kwa sasa.

Tunazo changamoto kadhaa, hii ndiyo sababu tunatakiwa kuweka bidii, kurekebisha makosa yaliyojitokeza,ili tutafute pointi zaidi kwenye michezo ijayo, tutaongeza nguvu ya mazoezi kuimarisha kikosi chetu hii ni kwa sababu tunahitaji kutimiza lengo la kuwa sehemu ya tiu nne za juu mwisho wa msimu na nafasi bado tunayo alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *