KIJUSO : ULIKUWA MCHEZO MGUMU

IMG_9151(1)

KOCHA msaidizi wa Mbeya City Fc Mohamed Kijuso amesema ugumu wa mchezo na kushindwa kutumia nafasi zilizopatikana ndiyo sababu ya  kushindwa kupata matokeo kwa kikosi chake kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya  Sokoine jijini hapa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo,kocha Kijuso alisema  City ilifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi katika vipindi vyote viwili vya mchezo lakini   vijana walishindwa kuzitumia nafasi hizo ikiwemo mkwaju wa penati amaabayo mshambuliaji Zahoro Pazzi alishindwa kutumbukiza mpira kimiani.

Tulijitahidi sana tumetengenza nafasi nyingi tukashindwa kuzitumia, tumepata penati tuakosa wenzetu walipata nafasi kama hiyo wakaitumia kusawazisha mchezo, siwezi kuwalaumu wachezaji wangu huu ni mpira wa miguu kuna wakati unagoma hata kama umecheza vizuri, tunakubaliana ma matokeo kinachofuata sasa ni maandalizi kuelekea michezo iliyosalia, tunafahamu tunakwenda kucheza ugenini hivyo tuajindaa kwenda kupambana.

IMG_9154

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *