KATEPA: HATUNA HOFU MAY 14 NI YETU

dsc_0148

KIKOSI cha Mbeya City Fc,jioni ya leo kitaendelea na maoezi ikiwa ni maandalizi ya mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara dhidi ya Young Africans uliopangwa kuchezwa  jumapili ya May 14 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mbeyacityfc.com Meneja Geofrey Katepa amesema kuwa maandalizi kueleka mchezo huo wa May 14 yanaendelea vizuri  leo ikiwa ni siku ya nyingine ya mazoezi baada ya mapumziko siku ya jana kupisha sikukuu ya Mungano hapo jana.

Tulipumzika jana kupisha sikukuu ya Muungano, jioni  hii tunaendelea na mazoezi kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo ujao dhdi y Yanga,jambo muhimu kwa wapinzani wetu wajue kuwa tunakuja na kumejindaa vizuri, hatuna hofu yoyote juu yao huu ni mpira wa miguu, ndani ya dakika 90 timu yoyote inaweza kupata ushindi,hivyo wanapaswa kujindaa hasa hata kama watakuwa wanacheza nyumbani.

City inakutana na Yanga ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kupata ushindi  wa 2-1 kwenye mchezo wa duru ya kwanza uliochezwa  uwanja Sokoine jijini Mbeya, kwa mabao ya Hassan Mwasapile na nahodha Kenny Ally.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *