Daniel Mwakasungula – 90 dhidi ya Mbao.

1200X600

Tulicheza vizuri sana na kwa kasi ya hali ya juu sana. Tuliweza kumiliki mpira zaidi ya mpinzani wetu Mbao fc. Bado kuna changamoto hasa hasa kuanzia kwa kiungo mshambuliaji bado anashindwa kuwalisha mipira ya kutosha safu ya ushambuliaji, hii ilipelekea Frank Khamis awe anashuka chini kuja kutafuta mipira na hii ilipelekea walinzi wa Mbao wakiongozwa na Ndikumana pamoja na Yusuph Mgeta wawe Huru.

Licha ya kukosa penati timu ilitulia nakuendelea kucheza open football kwa kutanua uwanja lakini mipira bado ikawa haifiki kwa wakati kwa washambuliaji.

Mabeki wa  pembeni Hassan Mwasapili pamoja na John Kabanda  walitimiza majukumu yao ya msingi kwa kuweza kuzuia na kupandisha mashambulizi, na bado kuna shida kwa mabeki wakati ambao mara nyingi wamekosa mawasiliano kati yao.

Timu ipo vizuri na mwalimu ameweza kubadilisha maeneo mengi hasa hasa kimbinu na kiufundi; timu ina uwezo wa kupiga pass zaidi ya saba kwa kasi.

Imeandaliwa na

Daniel Mwakasungula
MCCFC TV
Mbeya

752-386-851

Daniel Mwakwasungula ni CEO wa EFF, On air personality na sports analyst.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *