CITY SAFARINI DAR ‘KUIVAA’ YANGA JUMAMOSI

mbeya city fc 250 x 150 copy

KIKOSI Mbeya City Fc , leo kinaanza safari kuelekea  jijini Dar  es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Young Africans uliopangwa  kuchezwa kwenye uwanja wa Uhuru  jumamosi hii.

Afisa habari wa kikosi  hiki  Dismas Ten  ameifahamisha  mbeyacityfc.com kuwa  jumla ya nyota  18 na viongozi  10 watakuwa  kwenye msafara  huo  kwa ajili ya kuhakikisha  City  inafanikiwa  kuibuka na pointi tatu muhimu  na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.

Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu, tunataka kushinda  na kupata matokeo muhimu  kwenye mchezo  wa jumamosi,tunafahamu Young Africans ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo halitupi  hofu kwa sababu sisi pia tuna kikosi kizuri, tulipata matokeo duru ya kwanza  na sasa tunakwenda Dar kuhitimisha  dhamaira yetu ya kupata poiti sita msimu huu kutika kwao

Akiendelea  zaidi Ten alisema City  imekuwa  na wiki nne za kujindaa vizuri kukabili Young Africans  kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki  ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea  Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru.

Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye uwanja wa Sokoine April 13,hivyo nguzu zetu zote tunaziweka siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru.


Download Hapa

Miongoni mwa nyota waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Mrisho Ngassa,Hassan Mwasapile,Tumba Lui na Zahoro Pazzi

Kwa upande wake kocha mkuu Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Young Africans hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi.

Sina wasiwasi,wakati huu ambao sikuwa na mchezo wa ligi nilikuwa nawafuatilia, najua mbinu zao na nimewandaa vijana wangu vizuri ni wazi tutashinda  tena dhidi yao kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa duru ya kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *