CITY MKOANI RUVUMA

1200X600 SE

Kikosi cha City kinachojumuisha nyota 21, benchi la ufundi, maafisa na watumishi wa kila siku wa klabu hii kipo mkoani Ruvuma kwa ajili ya michezo mbalimbali na vilabu vya mkoani hapa. Klabu yetu ilifika mkoani Ruvuma siku ya ijumaa tarehe 05 ya mwezi huu wa januari na kutia nanga katika pwani ya ziwa hapa Mbamba Bay.

Jumapili tulianza kucheza michezo mbalimbali na vilabu vinavyoshiriki ligi daraja la pili, na ligi ya mkoa. Mchezo wa kwanza ulitukutanisha na timu ya Tumbi na kuibuka na ushindi wa goli nne bila, mchezo uliofuata tukacheza na Mapendo SC na kushinda goli mbili bila. Siku ya Jumatatu tulicheza na Mkali Stars na kuibuka na ushindi wa goli tano bila. Sehemu ya timu hizi hapa mkoani Ruvuma zinaundwa na vijana machachari na nyota wachanga walio na kiu kubwa ya kufanikiwa katika soka, hivyo ujio wa City mkoani hapa ni hatua kubwa sana kwao kama wachezaji na vilabu.

Leo tarehe 09 Januari tunacheza na Mbinga United inayoshiriki ligi daraja la pili, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kutokana na timu hii kuwa na mashabiki wengi na soka safi mkoani hapa. Kama mipangilio itakua safi tunataraji kujifua na Majimaji SC hapo kesho katika uwanja wa Majimaji Songea mjini.

Baada ya kuwepo mkoani hapa, City itarejea nyumbani Mbeya tayari kukutana na Prisons SC ya Iringa, mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Imetolewa na

Shah Mjanja
Afisa Habari
MCCFC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *