BOMBI NYUMBII MAJIMAJI

1200X600 SE

Dakika 90 za raundi ya 16 mechi nambari 127 mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara zimemalizika kwa klabu yetu kupata alama 3 muhimu. Magoli yetu yakifungwa na Eliud Ambokile na Frank Hamisi, huku goli la kufutia machozi la Majimaji likifungwa na mshambuliaji wetu wa zamani Peter Mapunda.

Matokeo haya yanaifikisha City mpaka nafasi ya 7 kabla ya michezo mingine mitatu ya raundi hii kukamilika.

Baada ya mechi hii City itasafiri kwenda Mtwara kwa ajili ya mechi nambari 134 dhidi ya Ndanda FC katika dimba la Nangwanda Sijaona.

Video: Tazama kikosi cha City msimu wa 2014/15

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *