CITY YAVUNA ALAMA ZINGINE 3

1200X600

Goli pekee la mshambuliaji Eliud Ambokile jezi nambari 10 mgongoni limetosha kuipandisha City hadi nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania bara. Dakika ya 34 Eliud alitupia gozi la ng’ombe katika lango la Njombe Mji pasipo kupepesa macho, na goli hilo lilidumu hadi filimbi ya Mwamuzi ilipopulizwa kuashiria kumalizika kwa mchezo huo.

Eliud anaifungia City goli muhimu kwa mara ingine tena, baada ya goli lake la kwanza alilofunga katika mechi ya ufunguzi wa ligi; mchezo uliochezwa hapa Sokoine na City kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa sifuri dhidi ya Majimaji ya Songea.

Kikosi cha City kinarudi kambini kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Stand United tarehe 24.09.17 huko Shinyanga.

Shah Mjanja
Afisa Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *